Coart_of_arm

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

TANZANIA WILDLIFE RESEARCH INSTITUTE

Wildlife Research for Conservation

DKT. MJINGO ASHIRIKI UPANDAJI WA MITI 2030 WILAYA YA ARUSHA KUADHIMISHA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ashiriki katika zoezi la upandaji wa miche ya miti dawa 2,030 iliyopandwa katika shule ya Sekondari ya Mringa iliyoko Mkoani Arusha, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Modest Mkude amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Amosi Makala katika zoezi hilo na kuishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuendesha zoezi la uhifadhi wa Mazingira kwa kupanda miche ya miti dawa na kuitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuwapatia wanafunzi miche ya miti dawa ili wakaipande majumbani mwao.

Aidha Mhe. Mkude amesema kuwa kauli Mbiu ya siku wanyamapori Duniani ambayo ni “mimea dawa, na manukato: kutunza afya, kuhifadhi urithi na kuboresha maisha” ishara kubwa kuwa uhai wa binadamu unategemeana na maisha ya Wanyamapori.

Ameongeza kuwa uhifadhi wa Mazingira unatakiwa kutiliwa mkazo hasa kwa kizazi cha sasa ili mimea dawa iendelee kuwepo kwa ajili ya kizazi kijacho hivyo ni bora kuwafundisha vijana namna bora ya kuhifadhi mazingira kwa kutumia mimea dawa.

Aidha Mhe. Mkude alitembelea mabanda ya maonesho yaliyopo katika viwanja vya nanenane kwa kupata maelezo mbalimbali kutoka idara za wizara, Taasisi zilizo chini ya wizara na zile ambazo ziko nje ya wizara, pia na wadau wa Mimea Dawa.

Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Alex Lobora ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii alisema kuwa Wanyamapori wamekuwa wakitumia mimea tiba kabla ya bindamu hivyo mimea tiba inatusaidia kwenye kuhifadhi mazingira lakini pia ni tiba kwa binadamu na wanyama.