Coart_of_arm

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

TANZANIA WILDLIFE RESEARCH INSTITUTE

Wildlife Research for Conservation

NAIBU KATIBU MKUU-UTALII ATEMBELEA BANDA LA TAWIRI KATIKA KUELEKEA SIKU YA MAONESHO YA WANYAMAPORI DUNIANI

Naibu Katibu Mkuu-Utalii Bw. Nkoba E. Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh. Joseph Mkude Pamoja na wadau mbalimbali wametembelea Banda la TAWIRI katika Viwanja vya Nane Nane, Njiro – Arusha, kuelekea Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanyamapori Duniani 2026.

Ziara hii imeakisi dhamira ya Taasisi katika kuunga mkono kauli mbiu ya mwaka huu:
🌿 “MIMEA TIBA na DAWA: KUTUNZA AFYA, KUHIFADHI URITHI NA KUBORESHA MAISHA.”

Kupitia tafiti za kisayansi, elimu ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa rasilimali asilia, TAWIRI inaendelea kulinda bioanuwai na kuhamasisha matumizi sahihi ya mimea tiba kwa manufaa ya afya ya jamii, urithi wa Taifa na maendeleo endelevu.

TAWIRI – Kinara wa Tafiti na Uhifadhi kwa Maendeleo ya Vizazi vijavyo.

TAWIRI #SikuYaWanyamaporiDuniani2026 #MimeaTibaNaDawa #Uhifadhi