Ellen Ponsian, ni mwanamke mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), licha ya kuwa na umri chini ya miaka 30 anashiriki moja kwa moja katika ustawi wa mnyamapori mfalme wa nyika simba kupitia mradi wa utafiti wa Simba Serengeti.
Mradi wa Simba Serengeti ni miongoni mwa miradi ya kitafiti ya muda mrefu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambao unafuatilia idadi, tabia na mienendo ya makundi ya simba na kutoa taarifa za kisayansi zinazotumika kuimarisha uhifadhi wa Simba ambaye ni kivutio cha utalii.
Porini kwenye wanyamapori wakali ni moja ya Ofisi za mtafiti Ellen akishiriki katika zoezi la kuwatafuta simba, kuwafuatilia kwa kutumia vifaa maalum na wakati mwingine kushiriki katika operesheni za kuwakamata kwa muda ili kuwafunga mikanda ya visukuma mawimbi (GPS collars).
Aidha, Mradi wa Simba Serengeti unafuatilia makundi takribani 20 ya Simba ambapo wote hutambuliwa kwa madoa ya Kipekee kwenye uso eneo la ndevu (Whisker spots), alama nyinginezo za asili na kupewa kadi maalumu ya utambulisho kulingana na kundi husika .
Kupitia kazi inayohusisha kumkaribia mnyama hatari kama simba, mtafiti Ellen anaonyesha Umri na Jinsia sio kikwazo cha kiutendaji.











Users Last 7 days : 704
Users This Month : 753
Total Users : 66927