Coart_of_arm

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

TANZANIA WILDLIFE RESEARCH INSTITUTE

Wildlife Research for Conservation

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DKT. ASHATU KIJAJI AONGOZA ZOEZI LA KUWAFUNGA TEMBO VISUKUMA MAWIMBI.

Kuelekea siku ya Wanyamapori Duniani, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, yuko uwandani katika Pori la Akiba Mkungunero kuyafunga makindi ya Tembo Visukuma mawembi ili kufahamu muelekeo wao, kwa lengo la kuwazuia kuleta madhara kwa wananchi na mazao yao.

Zoezi hili pia ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba ya kuwadhibiti Wanyamapori wakali na waharibifu husani Tembo.

Dkt. Kijaji ameishukuru Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kutoa fedha za kununua Visukuma Mawimbi, ndege nyuki pamoja na kutoa fedha Kwa Wizara na Taasisi zake ili kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuhifadhi.