Coart_of_arm

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

TANZANIA WILDLIFE RESEARCH INSTITUTE

Wildlife Research for Conservation

Latest News & Updates

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbas ameitaja Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania ( TAWIRI ) kuwa ya kimkakati na umuhimu mkubwa katika sekta ya Maliasili na utalii ambapo tafiti za TAWIRI ni dira katika kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Akizungumza na wajumbe wa timu ya menejimenti wakati wa ziara katika taasisi hiyo , Dkt. Abbas amesema kipaumbele cha Wizara ya Maliasili na Utalii ni kuendelea kuhifadhi maliasili iliyopo kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Aidha, Dkt. Abbas ameeleza TAWIRI ni daraja muhimu kwa ustawi wa taasisi nyingine za uhifadhi kwa kutoa ushauri wa kitaalum kuhusiana na wanyamapori ” sekta ya uhifadhi inaitegemea TAWIRI kutoa mbinu bora zitakazo wezesha uhifadhi na ustawi wa wanyamapori na makazi yao”ameeleza Dkt.Abbas

Dkt. Abbas ametoa wito kwa Viongozi wa TAWIRI kuhakikisha umma unapata matokeo ya Tafiti za wanyamapori zinazofanyika ili kuzitumia kwa maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Ernest Mjingo amemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara na nakuahidi kupokea maelekezo yote kwa ajili ya utekelezaji.

Our Research Partners & Collaborators

TANAPA
TFS
WWF
FZS
NCAA
TAWA
TAFORI
MWEKA
WCS
SIX RIVERS