Coart_of_arm

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

TANZANIA WILDLIFE RESEARCH INSTITUTE

Wildlife Research for Conservation

Category: news

VIZIMBA VYAWANUSURU WANAWAKE NA WATOTO AMBAO WALIKUWA WAKISHAMBULIWA NA MAMBA KWA ASILIMIA 46.

Hali ya maisha ya kawaida imerejea kwa jamii ziishizo pembezoni mwa mito na maziwa baada ya Wizara ya Maliasili kupitia wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamopori Tanzania (TAWIRI) kujenga vizimba 50 katika maeneo mbalimbali nchini.

Wanawake na watoto ni wanufaika wakuu wa ujenzi huu wa vizimba, Elizabeti Majaliwa mkazi wa mguluma amesema awali waliishi kwa hofu ya kushambuliwa na mamba wakati wa kuteka maji kwa shughuli za nyumbani. Pia watoto walishambuliwa wakati wa kuogelewa ila kwa sasa wapo salama.

Mtafiti wa Mamba kutoka TAWIRI, Dkt. Iddi Lipende amesema, ujezi wa vizimba hivyo unalenga kuzuia/kupunguza athari za mamba katika jamii, hivyo kuimarisha usalama na ustawi wa jamii pamoja na kuwaifadhi mamba.

Dkt.Lipende amebainisha kwa mujibu wa utafiti wa Mwaka 2018, katika migongano kati ya binadamu na mamba Wanawake na Watoto ni waathirika wa mashambulio kwa asilimia (46-47%), wanaume huathirika kwa asilimia 11 kutokaa na shuguli za Uvuvi na asilimia 58 ya madhara ya mashambulio ya Mamba ni kifo huku wanao okolea kupata ulemavu wa kudumu.

Read More »

MAADHIMISHO YA SIKU YA MISITU DUNIANI NA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KITAIFA

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ni miongoni mwa Taasisi zitakazo shiriki Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Kampeni ya Upandaji Miti Kitaifa yatakayofanyika kuanzia tarehe 18 Hadi 21, Machi 2026 katika Viwanja vya Ilulu Mkoani Lindi.

TAWIRI inawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kuja kupata elimu juu ya tafiti za wanyamapori pamoja na makazi yao ikiwemo misitu.

Read More »

UMRI MDOGO HAUMZUII KUWASHIKA SIMBA TAYA PORINI

Ellen Ponsian, ni mwanamke mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), licha ya kuwa na umri chini ya miaka 30 anashiriki moja kwa moja katika ustawi wa mnyamapori mfalme wa nyika simba kupitia mradi wa utafiti wa Simba Serengeti.

Mradi wa Simba Serengeti ni miongoni mwa miradi ya kitafiti ya muda mrefu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambao unafuatilia idadi, tabia na mienendo ya makundi ya simba na kutoa taarifa za kisayansi zinazotumika kuimarisha uhifadhi wa Simba ambaye ni kivutio cha utalii.

Porini kwenye wanyamapori wakali ni moja ya Ofisi za mtafiti Ellen akishiriki katika zoezi la kuwatafuta simba, kuwafuatilia kwa kutumia vifaa maalum na wakati mwingine kushiriki katika operesheni za kuwakamata kwa muda ili kuwafunga mikanda ya visukuma mawimbi (GPS collars).

Aidha, Mradi wa Simba Serengeti unafuatilia makundi takribani 20 ya Simba ambapo wote hutambuliwa kwa madoa ya Kipekee kwenye uso eneo la ndevu (Whisker spots), alama nyinginezo za asili na kupewa kadi maalumu ya utambulisho kulingana na kundi husika .

Kupitia kazi inayohusisha kumkaribia mnyama hatari kama simba, mtafiti Ellen anaonyesha Umri na Jinsia sio kikwazo cha kiutendaji.

Read More »