Coart_of_arm

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

TANZANIA WILDLIFE RESEARCH INSTITUTE

Wildlife Research for Conservation

Category: news

RAIS SAMIA APOKEA TAARIFA YA SENSA YA WANYAMAPORI, APONGEZA MAFANIKIO YA UHIFADHI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amepokea Taarifa ya Sensa ya Wanyamapori ya Taifa ya Mwaka 2024/2025 iliyowasilishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Ikulu, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Dkt. Samia ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na TAWIRI kwa kufanikisha zoezi hilo kubwa la kitaifa, ambalo kwa mara ya kwanza limefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali.

Rais Dkt. Samia amesema matokeo ya sensa hiyo yanaonesha mafanikio makubwa ya juhudi za uhifadhi nchini na kuthibitisha kuwa Tanzania inaendelea
kuwa miongoni mwa mataifa yenye utajiri mkubwa wa
wanyamapori duniani.

Aidha, Rais ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali za asili ili Watanzania waone thamani ya urithi huo wa taifa na kushiriki kikamilifu katika kuutunza kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Pia amesisitiza umuhimu wa kuwajengea watoto na vijana uelewa wa wanyamapori wa Tanzania kwa kuwafundisha majina yao ya Kiswahili na kuimarisha utamaduni wa kuthamini urithi wa taifa tangu wakiwa wadogo.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha utekelezaji wa sensa hiyo kwa kutenga fedha za ndani, hatua iliyowezesha Tanzania kufanya sensa ya kitaifa ya wanyamapori kwa kutumia rasilimali zake wenyewe.

Amesema sensa hiyo, ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10, inalenga kubaini idadi, mtawanyiko, mwenendo na hali ya ustawi wa wanyamapori pamoja na changamoto zinazoweza kuathiri mifumo ya ikolojia na sekta ya utalii.

Matokeo ya sensa iliyofanyika kati ya Septemba 2024 na Oktoba 2025 yanaonesha uwepo wa spishi 28 za wanyamapori wa kati na wakubwa katika mifumo mbalimbali ya ikolojia nchini. Kwa ujumla, matokeo yanaonesha mwenendo chanya wa uhifadhi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Aidha, matokeo ya kina ya sensa hiyo yanatarajiwa kutangazwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii.

Read More »

VIZIMBA VYAWANUSURU WANAWAKE NA WATOTO AMBAO WALIKUWA WAKISHAMBULIWA NA MAMBA KWA ASILIMIA 46.

Hali ya maisha ya kawaida imerejea kwa jamii ziishizo pembezoni mwa mito na maziwa baada ya Wizara ya Maliasili kupitia wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamopori Tanzania (TAWIRI) kujenga vizimba 50 katika maeneo mbalimbali nchini.

Wanawake na watoto ni wanufaika wakuu wa ujenzi huu wa vizimba, Elizabeti Majaliwa mkazi wa mguluma amesema awali waliishi kwa hofu ya kushambuliwa na mamba wakati wa kuteka maji kwa shughuli za nyumbani. Pia watoto walishambuliwa wakati wa kuogelewa ila kwa sasa wapo salama.

Mtafiti wa Mamba kutoka TAWIRI, Dkt. Iddi Lipende amesema, ujezi wa vizimba hivyo unalenga kuzuia/kupunguza athari za mamba katika jamii, hivyo kuimarisha usalama na ustawi wa jamii pamoja na kuwaifadhi mamba.

Dkt.Lipende amebainisha kwa mujibu wa utafiti wa Mwaka 2018, katika migongano kati ya binadamu na mamba Wanawake na Watoto ni waathirika wa mashambulio kwa asilimia (46-47%), wanaume huathirika kwa asilimia 11 kutokaa na shuguli za Uvuvi na asilimia 58 ya madhara ya mashambulio ya Mamba ni kifo huku wanao okolea kupata ulemavu wa kudumu.

Read More »