KATIKA MAONESHO KARIBU-KILI FAIR 2024, TAWIRI TUNATOA USHAURI ELEKEZI WA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UTALII (CONSULTANT)

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ni Miongoni mwa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii zinazoshiriki maonesho ya Karibu KILI FAIR 2024 yanayoendelea katika viwanja vya Kisongo, Magereza Mkoani Arusha.

Maonyesho haya ya KARIBU KILI FAIR 2024 yamejikita kuendelea kukuza na kuimarisha Utalii ambapo yanakutanisha zaidi ya Makampuni 700 ya Kimataifa kutoka takribani Mataifa 50 na Makampuni wenyeji zaidi ya 500 ikiwa ni fursa kwa Wadau wa utalii kutangaza huduma pamoja na kubadilishana uzoefu na makampuni mengine ya ndani na nje ya nchi.

Aidha, Maonesho haya KARIBU KILI FAIR yameanza katika Viwanja vya Kisongo- Magereza Jijini Arusha ikiwa ni jukwaa maalumu la kuyaweka pamoja makampuni ya ndani na nje ya nchi yanayohusika na sekta ya Utalii na wadau wengine wa utalii.

TAWIRI tunawakaribisha wadau kupata elimu juu ya mchango wa tafiti za wanyamapori katika kukuza utalii na tunatoa ushauri wa kitaalamu (consultancy) wa uwekezaji kwenye utalii, uanzishaji wa mashamba ya wanyamapori (Zoo), matibabu ya wanyamapori pamoja, ufugaji bora wa nyuki na huduma mahususi ya kutoa elimu ya kisayansi juu ya wanyamapori (Scientific talks)

Vilevile ,tunawakaribisha wadau kuja kuona fursa zilizopo kwenye tafiti na namna wanaweza kushiriki na TAWIRI ili kuwa na uhifadhi endelevu wa utajiri wa rasilimali ya wanyamapori na kukuza utalii nchini

KARIBU KILI FAIR 2024, TAWIRI tupo banda la Maliasili na Utalii tembelea tukuhudumie .

Visitors

021564
Users Today : 25
Users Last 7 days : 535
Users This Month : 1747
Total Users : 21564

Office Location

Contact Us